Watu wanne wauwawa kwenye shambulizi la bomu | Habari za Ulimwengu | DW | 22.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Watu wanne wauwawa kwenye shambulizi la bomu

Mshambulizi wa kujitoa muhanga maisha amejilipua karibu na kituo cha upekuzi cha polisi na jeshi la Irak katika wilaya ya Ghazaliya, magharibi mwa mji mkuu Baghdad hii leo.

Duru za polisi zinasema watu wanne wameuwawa na wengine sita wamejeruhiwa katika hujuma hiyo. Miongoni mwa waliouwawa ni mwanajeshi wa Irak, lakini maiti nyengine tatu zimeungua kiasi cha kutoweza kutambulika.

Machafuko yamepungua nchini Irak katika miezi michache iliyopita, lakini maafisa wa polisi na wanajeshi bado wanalengwa mara kwa mara na washambuliaji wa kujitoa muhanga maisha katika baadhi ya sehemu za Baghdad na mikoa ya kaskazini mwa mji huo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com