Watu wanane Kisiwani Pemba wakamatwa kwa kuwasilisha barua Umoja wa Mataifa
13 Mei 2008Matangazo
Pia watu wengine 4 wamekwenda mafichoni wakiogopa kukamatwa. Hayo yanatokana na taarifa waliopeleka Umoja wa Mataifa kutaka mfumo wa Shirikisho kwa Serikali ya Zanzibar.
Othman Miraji alizungumza na Hamad Ali Musa, mmoja wa watu kutoka Pemba anayedai yuko mafichoni Dar es salaam akiogopa kukamatwa na ni kati ya wale watu waliotoa takwa la kuwa na serikali ya Shirikisho.
Anaelezea hivi kuhusu mkasa huo.◄