1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 40 wauwawa kwenye shambulio la kujitoa muhanga

3 Machi 2008

-

https://p.dw.com/p/DGkz

PESHAWAR

Mshambuliji wa kujitoa muhanga amejirupua miongoni mwa maelfu ya wanachama wa makundi ya kikabila waliokuwa wakijadiliana juu ya kuyapinga makundi ya Alqaeda na Taliban nchini Pakistan. Shambulio hilo lililotokea kaskazini magharibi mwa nchi limesabisha kuuwawa kwa watu 40.

Kuongezeka kwa mashambulio hayo kunaonyesha jinsi gani rais Pervez Musharraf alivyodhoofika katika kulidhibiti eneo hilo licha ya kutuma maelfu ya wanajeshi kupamabana na wanamgambo wakiislamu.

Hapo jana wanachama hayo wa makundi matano ya kikabila walikuwa wakijadiliana juu ya kukamilisha azimio ambalo litatoa nafasi ya kuadhibiwa kwa mtu yoyote anayewahifadhi au kuwasaidia wanamgambo hao wakiislamu wakiwemo wapiganaji wa kitaliban na Al Qaeda.