Wataalam wa kupambana na Ugaidi wakutana Ubelgiji | Matukio ya Kisiasa | DW | 28.07.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Wataalam wa kupambana na Ugaidi wakutana Ubelgiji

Wataalam wa kupambana na ugaidi wa Umoja wa Ulaya na Norway wanakutana Brussel kutafuta ufumbuzi wa kuzuia vitendo vya mauaji ya halaiki kama yaliyotokea hivi karibuni huko Oslo, nchini Norway ambapo watu 76 wameuwawa.

default

Mtuhumiwa wa ugaidi Anders Behring Breivik, aliyeketi kushoto

Mwanadiplomasia ambae alizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina, aliliambia shirika la habari la ufaransa AFP kwamba Poland ambayo kwa hivi sasa inashikilia uwenyekiti wa Umoja wa Ulaya ndiyo iliyoitisha mkutano huo.

Mkutano huo maalum, pamoja na mambo mengine utahusisha kupena taarifa miongoni mwao.

Mwanadiplomasia mwingine kutoka Umoja wa Ulaya alisikika akisema " hakuna kitakachoweza kuzuia uwendawazimu huu" huyu nae hakutaka jina lake liandikwe kwenye vyombo vya habari.

Norwegen nach den Anschlägen in Oslo und Utøya

Waombolezaji waliokusanyika katika jengo la halmashauri ya jiji la Oslo

Norway sio mwanachama wa Umoja wa Ulaya lakini ni sehemu ya matafia 25 ya mapatano ya mipaka huru ya eneo la Schengen.

Wataalamu wa kupambana na ugaidi wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kupata taarifa za kina za muuaji Anders Behring Breivick .

Tayari Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Jens Stoltenberg alitangaza kufanyika kwa uchunguzi huru kufuatia mauwaji hayo yaliyofanyika wiki iliyopita yaliyosababisha kiasi ya watu 76 kupoteza maisha.

Pamoja na ukosoaji anaokabiliana nao, Stoltenberg amesisitiza ukweli wa mkasa huo utapatikana. Tayari polisi imekwisha sema kwamba ilichelewa kufika katika eneo la tukio kutokana na kutokuwepo kwa helkopta ya kuwafikisha katika kisiwa hicho.

Polisi ilichelewa kwa kiasi cha saa nzima baada ya kupewa taarifa za kutokea kwa tukio hilo. sakati hilo liliongezeka kuwa kubwa zaidi pale ambapo polisi walipoomba boti mbili za kiraia kwenda katika kisiwa hicho baada ya kwao kubainika kuwa na matatizo ya injini.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Waziri Mkuu wa Norway alitangaza kuunda tume huru ya uchunguzi ambayo pia itaonesha hali halisi na la tukio hilo na kuelekeza kipi kilichokosekana na kipi kifanyike.

Aidha Stoltenberg pia alitangaza kuwepo kwa siku ya kuwakumbuka waliouwawa katika tukio hilo katika kisiwa cha Utoeya na katika mripuko katika ofisi za serikali katikakati ya jiji la Oslo.

Hata hivyo tarehe rasmi ya siku ya kumubukumbu bado haijatajwa. Lakini pia Waziri Mkuu huyo aliahidi kutoa fedha kufidia gharama za mazishi kwa familia za wafiwa wa tukio hilo kubwa kuwahi kutokea nchini Norway tangu vita vya pili vya dunia.

Mwandishi: Sudi Mnette/AFP
Mhariri:Abdul-Rahman

DW inapendekeza

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com