Maombolezi nchini Norway | Matukio ya Kisiasa | DW | 24.07.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Maombolezi nchini Norway

Wakati wananchi wa Norway wanaendelea kuomboleza vifo vya watu 92, vilivyotokea kwenye shambulio la bomu na ufyatuaji risasi, mshukiwa mkuu katika mashambulio hayo mawili anasemekana kukiri kuhusika kwake

default

Moshi unaonekana kutoka katikati mwa mji wa Oslo

Wakili wa mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 32, aliyetambulishwa kuwa mkristo wa mrengo wa kushoto, amekiambia kituo cha televisheni nchini Norway, NRK, kuwa mteja wake alisema alipanga mashambulio hayo katika muda wa kipindi kirefu.

Doppelanschlag Norwegen - Anders Behring Breivik

Mshukiwa mkuu wa shambulio la Norway

Mashahidi wanasema mwanamume huyo alijihami kwa bunduki na alivalia sare ya polisi na alifyatuwa risasi kwa watu waliokuwa wamepiga kambi katika kisiwa kimoja cha mapumziko, kaskazini magharibi mwa mji wa Oslo. Wengi wa wahanga hao walikuwa ni vijana. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi habari, waziri mkuu Jens Stoltenberg, amesema mauaji hayo ya halaiki yalikuwa mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo tangu vita vya pili vya dunia.

Mapema siku ya Ijumaa, kiasi ya watu 7 walifariki katika mripuko unaoshukiwa kuwa wa gari, katikati mwa mji wa Oslo, unaofikiriwa kutekelezwa na mwanamume huyo huyo.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel hapo jana alilaumu kile alichokiita 'chuki dhidi ya watu wengine' kuwa ni uwezekano wa sababu ya shambulio baya lililofanyika nchini Norway. Merkel alitoa risala zake kwa wananchi wa Norway na alimpigia simu waziri mkuu wa nchi hiyo, Jens Stoltenberg, baada ya mripuko huo.

Tote und Verletzte bei Explosion in Regierungsviertel in Oslo

Waziri mkuu wa Norway, Jens Stoltenberg

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle amesema Ujerumani itatoa usaidizi wake katika uchunguzi wa kiteknolojia wa uhalifu huo, na vilevile kuwashughulikia wahanga.

Umoja wa Ulaya ulieleza kushutushwa kwake kuhusu kile ulichosema kuwa ni shambulio ovu katika nchi inayosifika kwa jitihada zake za amani. Rais wa Marekani Barack Obama alitoa risala zake binafsi kwa watu wa Norway.

Mwandishi: Maryam Abdalla/dpa, afp
Mhariri: Kitojo Sekione.

DW inapendekeza

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com