1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Benny Gantz

Benjamin Gantz ni mwanajeshi wa Israel na mwanasiasa. Alihudumu kama mkuu wa 20 wa majeshi ya Israel kuanzia 2011 hadi 2015. Desemba 2018 alianzisha chama kipya kwa jina la Israel Resilience.

Chama chake baadae kiliungana na vyama vya Talem an Yesh Atid na kuunda muungano wa Blue and White. Muungano wa Gantz wa Blue and White unajumuisha kuweka ukomo wa mihula kwa nafasi ya waziri mkuu, kuwapiga marufuku wanasiasa walioshtakiwa katika bunge la Knesset , kuzifanyia marekebisho sheria za taifa la Israel kujumlisha jamii za wachache, kupunguza mamlaka ya kiongozi wa baraza la kidini kuhusu masuala ya ndoa, kuwekeza katika elimu ya mapema, kupanua huduma za afya, na kuingia tena katika mazungumzo na Wapalestina kwa ajili ya makubaliano ya amani. Ukurasa huu unakusanya maudhui za DW kuhusu Benny Gantz na chama chake cha Blue and White.

Onesha makala zaidi