Wasudan wa kusini na kaskazini wapambana
10 Oktoba 2010Matangazo
Waandamanaji hao walitoa mwito huo kwenye mkutano ulioitishwa na serikali kuunga mkono umoja wa taifa katika mji mkuu Khartoum. Kiasi ya watu 3,000 walikusanyika karibu na makao rasmi ya rais kwa mkutano huo,hivi sasa ikiwa ni miezi mitatu kabla ya kupigwa kura ya maoni. Katika kura hiyo wakaazi wa kusini ya Sudan wataamua iwapo eneo hilo la kusini linataka kujitenga au kubakia sehemu ya Sudan iliyoungana.
Mkutano huo umefanywa mjini Khartoum, wakati ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ulioongozwa na balozi wa Marekani Susan Rice ulikuwa ukikamilisha ziara yake ya siku nne nchini Sudan. Hali ya mvutano imezidi kati ya kaskazini na kusini ya Sudan kabla ya kupigwa kura ya maoni tarehe 9 Januari.