WASHINGTON: Usalama wa Iraq kujadiliwa ana kwa ana
18 Mei 2007Matangazo
Marekani na Iran zinataka kuzungumza ana kwa ana tarehe 28 mwezi huu.Majadiliano hayo yatahusika na hali ya usalama nchini Iraq.Mkutano huo unatazamiwa kufanywa mjini Baghdad.Hayo yatakuwa majadiliano ya kwanza ya ngazi ya juu kupata kufanywa kati ya pande hizo mbili,tangu miaka kadhaa.Serikali ya Washington inaituhumu Teheran kuwa inawasaidia wanamgambo wa madhehebu ya Kishia nchini Iraq,lakini Iran inakanusha lawama hizo.