1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Seneti kupiga kura kuhusu uamuzi wa Bush kuongeza vikosi Irak

17 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRD

Seneti ya Marekani inakutana hii leo kujadili azimio linalopinga uamuzi wa Rais George W.Bush kupeleka wanajeshi zaidi wa Marekani nchini Irak. Hiyo jana,Baraza la Wawakilishi linalodhibitiwa na chama cha Demokratik,lilipitisha azimio hilo kwa kura 246 dhidi ya 182.Hata wabunge 17 wa chama cha Bush cha Republican waliunga mkono azimio hilo.Lakini katika Seneti,Wademokrats wana wingi mdogo tu.Bush anataka kupeleka wanajeshi wengine 21,500 kusaidia kurejesha usalama nchini Irak.Tangu uvamizi wa Irak ulioongozwa na Marekani hapo mwezi Machi mwaka 2003,zaidi ya wanajeshi 3,100 wa Kimarekani na maelfu kwa maelfu ya Wairaki wameuawa.