wanasiasa wa Ujerumani waustaajabia uamuzi wa Uswissi | Matukio ya Kisiasa | DW | 01.12.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

wanasiasa wa Ujerumani waustaajabia uamuzi wa Uswissi

Uamuzi wa Uswissi juu ya minara ya misikiti wasikitikiwa.

Sebastian Edathy, mbunge wa Chama cha SPD cha Ujerumani

Sebastian Edathy, mbunge wa Chama cha SPD cha Ujerumani

Matokeo ya kura ya maoni huko Uswissi hapo juzi, jumapili, ambapo wengi wa wananchi walipinga kujengwa minara ya misikiti katika nchi hiyo ni jambo ambalo limezusha mshangao na wasiwasi. Umoja wa Mataifa unataka kuchunguza kama uamuzi huo unaambatana na Hati ya Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu. Na huko Uholanzi, kuna alama za kupaliliwa chuku dhidi ya Uislamu kutokana na uamuzi huo. Hapa Ujerumani watu wanastaajabu juu ya mgeuko huu katika Uswissi, nchi ambayo ina demokrasia ya kimsingi, yaani maamuzi huchukuliwa na wananchi moja kwa moja.

Nini kilichowapata wananchi wa Uswissi? Hili ni suali linaloulizwa kichinichini kutokana na matamshi ambayo mtu anayasikia baada ya kutolewa matukeo ya kura ya maoni ya wananchi huko Uswissi, wengi wao walipinga kujengwa minara katika misikiti ya nchi hiyo.

Hapa Ujerumani, mwanasiasa wa chama cha upinzani cha Social Democratic, SPD, anayeshughulikia masuala ya siasa za ndani, Sebastian Edathy, amestaajabu:

"Smjuwi Mswissi binafasi, lakini hadi sasa nilikuwa na picha nzuri, na naamini pale mtu anapoziangalia tarakimu, ataona haingii akilini vipi uamuzi huu umefikiwa. Wazi ni kwamba huko Uswissi kuna Waislamu wengi walio na siasa za wastani, wengi wao wakitokea eneo la Balkan. Kwa hivyo huo ni uamuzi ambao hauwezi kuelezeka kwa kutumia akili."

Katika baadhi ya sehemu za mashambani, hadi asilimia ya wapiga kura walipinga kujengwa minara ya misikiti. Sifa ya Uswissi imepungua sana, alisema msemaji wa wabunge wa Chama cha Kijani hapa Ujerumani anayeshughulikia masuala ya makanisa, Josef Winkler. Yeye anauona uamuzi huo kuwa ni mbaya sana, ni ishara kwa Waislamu kuambiwa : katikati ya Ulaya Wakristo wanaruhusiwa kila mahala kuonekana, lakini Waislamu, kwa hisani zenu, mjifiche na ikiwa mna majengo ya kukuwakilisheni basi kwa vyovyote yaisiwe kama vile mnavotaka, lakini iwe kama vile wanavotaka watu wengine.

Ishara hiyo imewafikia Waislamu. Nadeem Elias wa Baraza kuu la Waislamu la hapa Ujerumani:

"Tumeshtuka kutokana na uamuzi wa kura hiyo ya maoni ya wananchi wa Uswissi, hasa katika nchi inayojulikana kwa kutoelemea upande wowote na kuheshimu misingi ya sheria."

Nadeem Elias anahofia kwamba uamuzi huo utamuimarisha yule yeyote ambaye anauopinga Uislamu. Anasema hapa si suala la kuwa na hofu kwa Uislamu, lakini hapa ni suala la kuuchukia Uislamu, na kwamba uamuzi huo utaleta chuki ambayo huenda zikaamsha nguvu zilizo dhidi ya Uislamu.

Umauzi huu wa Uswissi umezusha mdahalo mkali hapa Ujerumani. Mwanasiasa wa chama cha CDU, Wolfgang Bosbach, mwenyekiti wa kamati ya mambo ya ndani katika Bunge la Ujerumani, pia anaiona hofu inayozidi miongoni mwa wananchi kuhusu Uislamu katika jamii, na kwamba tukeo la Uswissi litiliwe sana maanani. Kimsingi, kuweko mazungumzo juu maelezo zaidi ya ujenzi wa misikiti.

Lakini Hartfried Wolff, msemaji wa Chama cha FDP kuhusu haki za raia wa kigeni, anasema haina maana kwa namna yeyote kuingia katika mazungumzo ya kimsingi. Hiyo ina maana ni kuweka wazi kabisa kwamba mazungumzo juu ya ujenzi wa misikiti yasionekaqne kama upinzani dhidi ya Uislamu. Lakini, kwa upande mwengine, lazima iwe wazi pia kwamba uhuru wa dini maana yake pia mtu lazima aweze kutekeleze dini yake ndani ya mipaka ya katiba ya Ujerumani.

Lakini umuhimu wa maingiliano na Waislamu ni jambo linalowashughulisha wanasiasa wa Ujerumani na zaidi hali hiii iliochipuka ya mtindo wa Kiswissi. Uamuzi umefikiwa katika kura isiokuwa ya kidemokrasia, lakini umefikiw ana wananchi. Mwanasiasa wa chama cha CDU, Siegfried Kauder anasema mtu lazima atilie maanani hofu ya wananchi, kwa hivyo haifai kuitunga dola ya kisasa kama vile walivyofanya sasa watu wa Uswissi. Siegfried anasema Waswissi wamepata mbinyo mkubwa kutokana na tatizo la demokrasia yao inayotegemea kura ya maoni ya wananchi.

Mwandishi:Kiesel Heiner/ZR/ Miraji ,Othman

Mhariri:Abdul-Rahman

 • Tarehe 01.12.2009
 • Mwandishi Miraji Othman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/KnC4
 • Tarehe 01.12.2009
 • Mwandishi Miraji Othman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/KnC4
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com