Wananchi wa Nigeria leo kuwachagua wabunge | Matukio ya Kisiasa | DW | 02.04.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Wananchi wa Nigeria leo kuwachagua wabunge

Wanigeria leo wanapiga kura kuchagua bunge jipya katika mfululizo wa chaguzi zitakazofanyika hadi Aprili 16.

default

Wananchi wa Nigeria wakipiga kura

Uchaguzi huu mkuu ni jaribio la kuona iwapo nchi hiyo yenye watu wengi kabisa barani Afrika inaweza kuachana na historia ya uchaguzi wenye udanganyifu na vurugu.

Tume ya Uchaguzi ina matumaini kuwa daftari jipya la wapiga kura, taratibu imara za kupiga kura na usalama bora zitasaidia kukomesha udanganyifu, lakini tayari kulikuwa na ghasia katika mikoa kadhaa wakati wa kipindi cha kampeni.

Nigeria Ibrahim Shekarau und Nuhu Ribadu

Baadhi ya wagombea wa urais Nigeria, Ibrahim Shekarau, (shoto) na Nuhu Ribadu

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Nigeria, Attahiru Jega amesema kuwa miaka 12 iliyopita, nchi hiyo ilirejea katika utawala wa kidemokrasia na ilianza safari ambayo wengi walitarajia sasa itakuwa imeleta mfumo thabiti wa kidemokrasia lakini yasikitisha kuwa bado haijafikia hali hiyo.

Mipaka ya nchi hiyo ilifungwa kabla ya uchaguzi huo kuanza hii leo na maafisa wa uchaguzi, vikosi vya usalama na wafanyakazi wa dharura pekee ndio wanaoruhusiwa kusafiri katika barabara wakati wa saa za kupiga kura.

Mwandishi: Grace Patricia Kabogo (RTRE)
Mhariri: Prema Martin

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com