Wanajeshi wa Israel wazikwa na Hezbollah watoa heshima kubwa kwa wanamgambo na wapiganaji 199 | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 17.07.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Wanajeshi wa Israel wazikwa na Hezbollah watoa heshima kubwa kwa wanamgambo na wapiganaji 199

Maiti 199 zafanyiwa Gwaride la heshima na wanamgambo wa Hezbollah

default

Kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah asema enzi za kushindwa zimekwisha''

Kundi la Hezbollah limefanya gwaride la heshima kwa ajili ya wapiganaji wake 199 waliouwawa na Israel ambao miili yao ilikabidhiwa jana chini ya mpango wa kubadilishana wafungwa ambapo pia wafungwa wengine watano wa Lebanon waliachiwa huru.

Maiti za walebanon zikiwa kwenye majeneza yaliyopambwa yalipitishwa kutoka barabara za mji wa Naqoura ulioko kusini mwa nchi hadi mji mkuu Beirut huku magari yaliyobeba maiti hizo yakisimama kila kijiji kuwapa nafasi waliojitokeza kutoa heshima za mwisho kurusha mawardi na mchele kwenye majeneza hayo.

Magari yote yalikuwa yameandikwa maneno ya kuwasifu marehemu hao kwamba ni watu waliokufa mashahid na mashujaa wa vita.

Magari yote hayo yalikuwa yamebandikwa picha kubwa ya aliyekuwa kamanda wa jeshi la Hezbollah Imad Mughniyeh aliyeuwawa na ambaye alihusika kupanga uvamizi wa mwaka 2006 uliosababisha kuwakama wanajeshi wawili wa Israel Regev na Goldwasser.

Miongoni mwa wapiganaji 199 waliouwawa na Israel kuna wanamgambo sabaa wa Hezbollah ilhali wengine wengi waliosalia ni wapalestina ambao walihusika kufanya mashambulio nchini Israel kati ya miaka 70 hadi 80 akiwemo pia Dalal al Mughrabi mtu anayetambuliwa na wapalestina kama shujaa na kuangaliwa na Israel kama gaidi mkubwa kutokana na kuliteka nyara basi moja la waisraeli mnamo mwezi Marchi mwaka 1978 na kusababisha vifo vya waisraeli 30.

Kusini mwa Beirut wafungwa watano walioachiwa huru akiwemo Samir Kuntar waliweka mashada ya maua kwenye kaburi la Mughniyeh.

Kuntar aliyepokelewa kwa heshima kubwa katika uwanja wa ndaege wa kimataifa mjini Beirut hapo jana na kwenye uwanja wa michezo wa kusini mwa Beirut amesema hajutii kuhusu mauaji aliyoyatekeleza.

Ubadilishanaji huo wa wafungwa umeonekana kuwa ushindi kwa Hezbollah katika macho ya wapinzani na wafuasi wa kundi hilo.

Hassan Nasrallah Kiongozi wa Hezbollah binafsi alijitokeza kuwakaribisha nyumbani wanamgambo hao watano waliochwa na Israel na mbele ya mkutano mkubwa wa hadhara akasema kwamba enzi za kushindwa zimemalizika.Maneno hayo yameonekana kutiliwa nguvu pia na rais Michele Suleiman ambaye yeye alisema wataitetea ardhi ya Lebanon kwa njia yoyote ile.

Kwa Upnde wa Waisraeli yalikuwa ni majonzi moja kwa moja katika mazishi ya wanajeshi wake wawili yaliyoonyosehwa moja kwa moja kwenye televisheni ya taifa.

Mjane wa Gold wasser mwanajeshi aliyeuwawa alikuwa na huzuni nyingi huku akibubujikwa na machozi alisema na hapa tunamnukulu'' nilitumai kwamba ntaamka siku moja na kusema ilikuwa ndoto tu,ndoto mbaya''Mwisho wa kunukulu mjane wa Goldwasser.

Ehud Goldwasser amezikwa kwenye makaburi ya kijeshi katika mji alikozaliwa wa Nahriya kaskazini mwa Israel Eldad Regev amezikwa makaburi ya kijeshi ya mji wa Haifa.

Waziri wa Ulinzi wa Israel na mkuu wa zamani wa jeshi Ehud Barak pia alikuweko katika mazishi yote.Alikuwa mnyonge na mwenye huzuni nyingi wakati akitoa buriani amesema na hapa nikimnukuu'' tulitaka kukukaribisha tena pamoja na mwenzako Eldad Regev.Tulitaka kuwakumbatia na kuwaona mkitabasamu lakini tunawasindikiza leo hii machozi ya kitudondoka huku mioyo yetu ikiwa mizito.Mwisho wa kumnuku waziri wa ulinzi wa Israel Ehud Barak.

Kwa upande mwingine Rais Shimon peres amesema wamejitoa muhanga ili kuhakikisha roho za wanajeshi wake wawili zinalazwa mahala pema na huo ndio wanaouita ushindi na kwa hilo Lebanon imejidhalilisha.Lakini pia amesema Israel ina majonzi makubwa kutokana na kuwapoteza wanajeshi wake .Maswahiba wakubwa wa Hezbollah Iran imepongeza hatua ya kuachiwa huru wanamgambo walebanon na kusema ni habari za kufurahisha ambazo zimetokana na mafanikio ya upinzani wa kiislamu wa kundi la Hezbollah na taifa la walebanon.Waziri wa mambo ya nje wa Iran Manoucher Mottaki amesema yote hayo ni kufuatia ujasiri wa muda mrefu wa walebanon na mataifa ya eneo hilo na tunaupongeza ushindi huu mkubwa kabisa.

 • Tarehe 17.07.2008
 • Mwandishi Saumu Mwasimba
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EeJp
 • Tarehe 17.07.2008
 • Mwandishi Saumu Mwasimba
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EeJp
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com