Wakaazi waliopewa hifadhi kwenye kambi za muda nchini Kenya warejeshwa makwao | Matukio ya Kisiasa | DW | 05.05.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Wakaazi waliopewa hifadhi kwenye kambi za muda nchini Kenya warejeshwa makwao

Nchini Kenya operesheni ya kitaifa ya kuwarejesha makwao wakaazi waliokuwa wakipewa hifadhi kwenye kambi za muda katika mkoa wa Bonde la Ufa imeanza rasmi hii leo.

Watu waliolazimika kuyahama makaazi yao baada ya vurugu za Uchaguzi nchini Kenya

Watu waliolazimika kuyahama makaazi yao baada ya vurugu za Uchaguzi nchini Kenya

Taarifa zinaeleza kuwa kumeundwa vituo 32 vya polisi kwa lengo la kudumisha usalama katika eneo hilo.Hatua hii inachukuliwa baada ya Rais Mwai Kibaki na waziri Mkuu Raila Odinga wote wakiandamana na Makamu wa Rais kuzuru eneo hilo mwishoni mwa mwezi uliopita.Hata hivyo baadhi ya waathirika wa ghasia za uchaguzi pamoja na wanaharakati na viongozi wa kidini hatua ya maridhiano ingepewa kipaumbele na kujumuisha wahusika wote.

Kutoka Nairobi Mwai Gikonyo anaarifu zaidi.


Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com