Wahariri wazungumzia hotuba ya Merkel umoja wa Mataifa | Magazetini | DW | 22.09.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Wahariri wazungumzia hotuba ya Merkel umoja wa Mataifa

Wahariri katika magazeti ya leo wamejishughulisha zaidi na mkutano wa umoja wa mataifa wa malengo ya maendeleo ya milenia na mjadala unaohusu udhibiti wa silaha nchini Ujerumani.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akihutubia kikao cha Umoja wa Mataifa kinachojadili malengo ya maendeleo ya Milenia.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akihutubia kikao cha Umoja wa Mataifa kinachojadili malengo ya maendeleo ya Milenia.

Wahariri katika magazeti ya leo wamejishughulisha zaidi na mkutano wa umoja wa mataifa unaoangalia malengo ya maendeleo ya milenia , pamoja na mjadala nchini Ujerumani unaohusu udhibiti wa silaha.

Tukianza na mada ya mkutano wa umoja wa mataifa kuhusu malengo ya maendeleo ya milenia, gazeti la Rhein - Neckar-Zeitung linaandika:

Msaada wa maendeleo ni lazima kutumika , ikiwa utapatikana na sio kuingia katika matumbo ya wakubwa. Msimamo huu wa serikali ya Ujerumani ni sahihi kabisa, ikitiliwa maanani kuwa ni fedha kutoka kwa walipa kodi, lakini pia ni wajibu wa dunia nzima kutoa misaada. Kipya katika hili ni kutokuwa na ufahamu. Na kwa kuwa ahadi iliyotolewa hapo kabla , kwamba Ujerumani itatoa kiasi cha asilimia 0,7 ya pato lake jumla la mwaka na hadi sasa ahadi hiyo haijatimizwa inaonekana kuwa ni unafiki. Dunia ingepata msaada kiasi gani iwapo kiwango hicho cha asilimia 0.7 kingewekezwa na Ujerumani, anauliza mhariri wa gazeti la Rhein -Neckar.

Gazeti la Neue Presse la mjini Hannover, likizungumzia mada hiyo , linaandika:

Ujerumani haipaswi kuangalia mbali zaidi. Tangu mwaka 1970, kulikuwa na lengo la kuongeza msaada wa maendeleo kwa asilimia 0.7 kutoka pato lake jumla la taifa, hadi sasa msaada huo uko katika kiwango cha asilimia 0.4. Ujerumani ni dhahiri kuwa imevunja ahadi yake, ya kuongeza msaada wake kwa asilimia 0.7 ifikapo mwaka 2015. Merkel anaongoza kwa nguvu zake zote huku kukiwa na makosa kadha. Ingekuwa ni nafasi nzuri ya kujitangaza kwa ajili ya kupata kiti katika baraza la usalama la umoja wa mataifa, iwapo Ujerumani ingetimiza wajibu wake katika mapambano dhidi ya njaa na umasikini duniani.

Nalo gazeti la Westfälische Nachrichten la mjini Münster linaandika:

Kansela wa Ujerumani jana amefanya kila juhudi , kuionyesha Ujerumani kama nchi yenye heba na mshirika wa kutoa misaada ya maendeleo , ambayo inataka kuchukua nafasi ya kuwajibika duniani. Lakini kuhusiana na suala hili hali haikuwa nzuri. Kuhusiana na lengo Ujerumani ililoweka kwamba ifikapo mwaka 2015, msaada wa maendeleo utaongezwa hadi kufikia asilimia 0.7, inabidi serikali ya Berlin iweke juhudi zaidi. Kwa mujibu wa mpango wa kansela Merkel binafsi wa kubana matumizi nchini mwake, mpango huo kufikiwa unaonekana kuwa si halisi.

Mada nyingine ni inazungumzia mjadala wa udhibiti wa silaha, baada ya mama mmoja kuwauwa watu kadha nchini Ujerumani. Gazeti la Schwarzwälder Bote linaandika.

Kwa mtazamo wa kuweka sheria ngumu zaidi dhidi ya umilikaji wa silaha, hilo halisaidii sana. Na pia msimamo wa kundi linalotetea kuwa na silaha unasikitisha. Kwa kuwa suala hilo lote halikuwekewa sheria sahihi. Kuna kitu fulani kinakosekana katika usajili wa silaha wenye kufanyakazi. Katika hilo , mmiliki wa silaha za michezo ,ni lazima ajihusishe kwa karibu na mchezo wenyewe. Pendekezo ni kwamba , silaha na risasi vitenganishwe katika uhifadhi wake, hili linaonekana kuwa linaweza kukubalika. Atakayepinga mjadala huu, hautakii mema mchezo wa kulenga shabaha.

Mwandishi : Sekione Kitojo / Inlandspresse

Mhariri : Mohammed Abdul Rahman

 • Tarehe 22.09.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/PJ4x
 • Tarehe 22.09.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/PJ4x