Viongozi wa nchi za Kiarabu kukutana Misri | Matukio ya Kisiasa | DW | 19.01.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Viongozi wa nchi za Kiarabu kukutana Misri

Viongozi wa nchi za Kiarabu wanakutana leo nchini Misri kujadiliana kuhusu biashara na maendeleo. Huo ni mkutano wao kwanza tangu kiongozi wa Tunisia, Zine El Abidine Ben Ali aondolewe madarakani wiki iliyopita.

default

Katibu Mkuu wa jumuiya ya nchi za Kiarabu, Amr Moussa

Wakati huo huo, Rais wa Tunisia, Foued Mebazaa na Waziri Mkuu, Mohammed Ghannouchi jana wamejiuzulu kwenye chama tawala katika hatua ya kutimiza matakwa ya wanasiasa wa upinzani na viongozi wa chama kikuu cha wafanyakazi.

Kituo cha televisheni ya taifa kimeripoti kuwa viongozi hao wamebakia katika nafasi zao kama rais na waziri mkuu. Mapema, mawaziri wanne walijiuzulu kutoka katika serikali ya mpito ya Waziri Mkuu Ghannouchi. Wizara muhimu zinaendelea kushikiliwa na wafuasi wa rais wa zamani, Ben Ali.

NO FLASH Tunesien Unruhen Ghannouchi Mbazaa Tunis Regierung

Rais wa mpito wa Tunisia, Foued Mebazaa (Kulia) akiwa na Waziri Mkuu Mohammed Ghannouchi

Utawala wake wa miaka 23 ulimalizika baada ya wiki kadhaa za maandamano kupinga viwango vya umasikini na ukosefu wa ajira nchini humo. Kwenye mji mkuu wa Tunis, jana polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji ambao wanataka kuvunjwa kwa chama tawala.

 • Tarehe 19.01.2011
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/zzQn
 • Tarehe 19.01.2011
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/zzQn

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com