Vilnius. Waziri amaliza ziara yake katika eneo la Baltic. | Habari za Ulimwengu | DW | 14.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Vilnius. Waziri amaliza ziara yake katika eneo la Baltic.

Katika kituo chake cha mwisho katika ziara yake ya mataifa ya eneo la Baltic , waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier amewasili katika mji mkuu wa Lithuania Vilnius.

Baada ya mazungumzo na wanasiasa waandamizi , Steinmeier ataweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu ya wahanga wa uovu uliofanywa na majeshi ya Ujerumani yalipoivamia Lithuania katika vita vikuu vya pili vya dunia.

Wanajeshi wa Ujerumani waliwauwa kiasi cha watu 100,000 , kiasi cha watu 70,000 walikuwa Wayahudi katika msitu wa Peneriai mwaka 1941. Ziara hiyo nchini Lithuania ilitanguliwa na ziara nyingine nchini Estonia na Latvia mapema wiki hii.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com