VFL Wolfsburg mabingwa wa Bundesliga 2009 | Michezo | DW | 25.05.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

VFL Wolfsburg mabingwa wa Bundesliga 2009

Bayern Munich makamo bingwa mara hii.

default

VfL Wolfsburg -mabingwa 2009+++

Wolfsburg wametoroka na taji lao la kwanza la Bundesliga mwishoni mwa wiki baada ya kuizaba Werder Bremen mabao 5-1.

Wingu la huzuni limetandaa kaskazini-mashariki mwa Uingereza baada ya timu 2 za eneo hilo :Newcastle United na Middlesbrough kuteremshwa daraja ya pili msimu ujao-

Katika Ligi ya Ufaransa-Girondins Bordeaux imepiga hatua moja zaidi kunyakuwa taji la ubingwa la Ufaransa baada ya kuilaza Monaco bao 1-0.

"Firimbi ya mwisho imelia VFL Wolfsburg ni mabingwa wapya wa Ujerumani mwaka 2009:"

Kocha alieleta maajabu hayo Felix Maghat akasema:

"Ni ndoto iliotimilia.Msimu msima tulitia fora na naweza kudai tumestahiki kutawazwa mabingwa."-

alisema Felix Magath ambae hadi Jumamosi alikua kocha wa mabingwa wapya VFL Wolfsburg na msimu ujao anakuwa kocha wa Schalke 04.Taji la ubingwa la Wolfsburg ni kilele cha mafanikio ya kocha Magath na timu yake ambayo mara tu kuanza duru ya pili ya msimu iliendelea kutamba tena mfululizo.

Taarifa kuwa Magath sasa anaiachamkono Wolfsburg ili kuwa kocha msimu ujao wa Schalke, yamkini kutazusha wasi wasi mabingwa hawa wapya watakapoiwakilisha Ujerumani msimu ujao katika Kombe la Ulaya na nyumbani Bundesliga.Lakini, Wolfsburg ina mizinga 2 mikali ya kujivunia-mbrazil Grafite nas mbosnia Edin Dzeko ambao kwa pamoja wamevunja rekodi ya Gerd Mueller na uli Hoeness wa bayern Munich ya kutia mabao mengi msimu mmoja.

Mabingwa hadi Jumamosi-Bayern Munich waliocheza mechi yao ya mwisho na Stuttgart Jumamosi wakiwa pointi 2 nyuma ya Wolfsburg, walimaliza mara hii nafasi ya pili na hivyo wamekata tiketi yao moja kwa moja ya Champions League-kombe la klabu bingwa barani Ulaya.hii inafuatia ushindi wao nyumbani jumamosi wa mabao 2-1 dhidi ya Stuttgart iliomaliza nafasi ya tatu ya ngazi ya Ligi.

Munich imeshaanza kupanga kwa msimu ujao.Imemchagua kocha mpya kujaza pengo la Jurgen klinsmann waliemtimua baada ya jahazi aliloliongoza kwenda mrama tangu katika Kombe la Taifa la ujerumani,Kombe la ulaya na mwishoe Bundesliga.kocha mpya ni mholanzi Van Gaal.

Stuttgart iliomaliza nafasi ya 3 itacheza katika duru ya kuania tiketi maalumu ya champions League wakati hertha Berlin na Hamburg zimeangukia katika Ligi mpya ya ulaya inayoanzishwa kuchukua nafasi ya Kombe la UEFA.Nini hatima ya Hoffenmhiem, timu ya kijiji kidogo iliozusha maajabu mwaka jana wakati ya duru ya kwanza ya msimu ?

Kocha wao Regnick alisema:

""Duru ya kwanza tulicheza m,aridadi ajabu na duru ya pili ya msimu tumejionea zupande wapili wa sura ya dimba."

Hoffenheim,ilianza kupepesuka baada ya kuumia kwa m,shambulizi wao hatari Vedad Ibisevic, Hoffenheim iliopanda daraja ya kwanza msimu huu tu, ilianza kuteremka chini.

Katika safu ya nyuma ya ngazi ya Ligi, Armenia Bielefeld na Karlsruhe zimeshukla daraja ya pili wakati Enegie Cottbus ina nafasi moja zaidi ya kubakia daraja ya kwanza:Itacheza wiki hii na Nuremberg ya daraja ya pili kuamua kati yao ni ipi inabaki au inapanda daraja ya kwanza.

Nje ya Bundesliga-Ligi za Uingereza,Spain na Itali zilikwishatawaza mabingwa wao tangu mwishoni mwa wiki iliopita.Uingereza mabingwa waliibuka wale wale wa zamani Manchester united yenye miadi jumatano hii na FC Barcelona kwa finali ya Kombe la klabu bingwa barani ulaya mjini Roma. Barcelona ni mabingwa wa Spian wakati Inter Milan pia ni wa Itali.Mwishoni mwa wiki hii,New castle United na Middlesbrough zimeteremshwa daraja ya pili.Middlesbrough ilizabwa mabao 2-1 na West ham United.Timu ya 3 kuzama daraja ya pili ni West Bromwich.

Kileleni Liverpool iliilaza Tottenham Hotspur kwa mabao 3-1.Chelsea imeangukia nafasi ya 3 kufuatia ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Sunderland.Manu iliotoroka na taji lao la 3 la ubingwa mfululizo,imeichapa Hull City bao 1:0

Muandishi:Ramadhan Ali/DPAE

Mhariri: M.Abdulrahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com