1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN wafuta ziara ya ujumbe wa kutathmini mpango wa amani Burundi

21 Aprili 2008

-

https://p.dw.com/p/DlMG

BUJUMBURA

Umoja wa mataifa umefutilia mbali ziara ya ujumbe wake wa kutathmini mpango wa amani nchini Burundi iliyokuwa iifanyike jana.Hatua hii imechukuliwa baada ya kuripotiwa siku tatu za mapigano kati ya waasi na wanajeshi wa serikali katika mji mkuu Bujumbura ambapo kiasi cha watu 26 waliuwawa.

Hata hivyo msemaji wa jeshi nchini Burundi Adolphe Manirakiza amesema hakuna mapigano yaliyoripotiwa kutokea hapo jana ambayo ilikuwa siku ya kuwasili kwa ujumbe huo wa Umoja wa mataifa ingawa hali ilikuwa ni ya wasiwasi.Mapigano yalizuka alhamisi wakati waasi wa kundi la FNL walipovurumisha makombora katika vituo vya serikali kwenye vitongoji vya mji mkuu Bujumbura jambo ambalo liliwalazimu wanajeshi kujibu mashambulio.Utekelezwaji wa mpango wa amani ulikwama baada ya waasi wa FNL kujitoa katika tume ya kusimamia usitishwaji mapigano wakiwalaumu wapatanishi kwa upendeleo.Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon amelaani mapigano hayo ya karibuni akisema yanachangia mateso tu kwa raia na kuhujumu utekelezwaji wa makubaliano ya amani ya septemba mwaka 2006.