1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Burundi

Burundi, rasmi Jamhuri ya Burundi ni nchi nyingine mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyozungukwa na nchi kavu, ikipakana na Rwanda, Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Burundi ni nchi ya milima na tambarare. Watu wa makabila ya Wahutu, Watutsi na Watwa wameishi nchini humo kwa miaka isiyopungua 500. Kwa zaidi ya miaka 200 Burundi ilikuwa falme huru. Mwanzoni mwa karne ya 20 Ujerumani iliitawala lakini ilikabidhiwa na Ubelgji baada ya kushindwa kwa Ujerumani katika Vita Kuu vya Kwanza vya Dunia. Wabelgji walizitawala Burundi na Rwanda kama makoloni ya Ulaya yakijulikana kama Ruanda-Urundi. Mwaka 2015 ulishuhudia machafuko makubwa ya kisiasa, wakati rais Pierre Nkurunziza alipoamua kuwania muhula wa tatu madarakani, jaribio la mapinduzi lililoshindwa. Burundi yenye wakaazi wengi na fursa ndogo imeshuhudia uhamaji wa raia wake wengi wanaotafuta fursa nje ya nje.

Onesha makala zaidi