Umoja wa Ulaya wasifu kuondolewa sheria ya hali ya hatari Pakistan | Habari za Ulimwengu | DW | 16.12.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Umoja wa Ulaya wasifu kuondolewa sheria ya hali ya hatari Pakistan

Brussels:

Umoja wa Ulaya umesifu uamuzi wa kubatilishwa sheria ya halai ya hatari nchini Pakistan.”Hatua hiyo ni muhimu katika kuirejesha nchi hiyo katika mfumo wa kidemokrasi-“amesema hayo muakilishi mkuu wa siasa ya nje wa Umoja wa Ulaya Javier Solana.Wakati huo huo mwanasiasa huyo wa umoja wa ulaya ameutolea mwito uongozi mjini Islamabad uhakikishe uchaguzi wa bunge unakua huru na wa haki.Uchaguzi huo wa bunge utaitishwa january nane ijayo.Marekani pia imesifu uamuzi wa kuondolewa sheria ya hali ya hatari.Jana rais Pervez Musharraf amebatilisha sheria hiyo aliyoitangaza mapema mwezi uliopita.Hata hivyo upande wa upinzani nchini Pakistan unaamini vyombo vya habari na vile vya kisheria vitaendelea kukaguliwa.Wanahoji hali hiyo itakorofisha kampeni huru ya uchaguzi.

 • Tarehe 16.12.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CcHG
 • Tarehe 16.12.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CcHG

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com