1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUbelgiji

Umoja wa Ulaya walaani uchaguzi wa Urusi ndani ya Ukraine

18 Machi 2024

Umoja wa Ulaya umelaani kufanyika uchaguzi kwenye maeneo ya Ukraine yanayokaliwa na Urusi.

https://p.dw.com/p/4drwn
Umoja wa Ulaya umesisitiza kuwa hautatambua uchaguzi wa Urusi kwenye maeneo ya Ukraine.
Umoja wa Ulaya umesisitiza kuwa hautatambua uchaguzi wa Urusi kwenye maeneo ya Ukraine.Picha: AP/picture alliance

Hatua hiyo imejiri baada ya kutangazwa kwamba rais wa Urusi ameshinda uchaguzi huo kwa kishindo.

Umoja wa Ulaya umesema katika tamko lake kwamba unalaani vikali uchaguzi huo katika jimbo la Crimea lililotekwa na Urusi mnamo mwaka 2014 kinyume cha sheria za kimataifa na pia kwenye majimbo ya Donetsk, Luhansk, Zaphorizhzhya na Kherson.

Jumuiya hiyo ya Ulaya imesisitiza kuwa haitatambua uchaguzi kwenye maeneo hayo au matokeo yake.

Mkuu wa masuala nje wa Umoja wa Ulaya Joseph Borrell, pia amesema kifo cha kushtusha cha mwanasiasa wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny kabla ya kufanyika uchaguzi ni ishara nyingine ya kuongezeka kwa mfumo wa ukandamizaji.