UMOJA WA MATAIFA–NEW YORK:Mustakabal wa Kosovo kucheleweshwa | Habari za Ulimwengu | DW | 21.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

UMOJA WA MATAIFA–NEW YORK:Mustakabal wa Kosovo kucheleweshwa

Marekani na washirika wake wa Umoja wa Ulaya katika
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wamesambaza
waraka wa azimio, litakalochelewesha mabadiliko
kuhusiana na hali ya baadae ya jimbo la Serbia la
Kosovo. Kucheleweshwa huko kwa siku 120 kunalenga kuruhusu mazungumzo yaanze kati ya Serbia na
viongozi wa jamii ya wenye asili ya Kialbania katika Kosovo kuhusu hali ya baadae ya jimbo hilo.

Serbia na
Urusi zinaupinga mpango wa umoja wa mataifa unaopendekeza uhuru kamili kwa Kosovo na Urusi imetishia kutumia kura ya turufu kupinga azimio litakalounga mkono uhuru kwa Kosovo.Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com