Umoja wa mataifa, New York. Venezuela na Guatemala zatoka sare umoja wa mataifa. | Habari za Ulimwengu | DW | 20.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Umoja wa mataifa, New York. Venezuela na Guatemala zatoka sare umoja wa mataifa.

Baada ya duru 13 za upigaji kura katika siku moja kushindwa kupata mshindi kati ya nchi ya Guatemala na Venezuela kuhusiana na kuichagua nchi mojawapo kati ya hizo kuingia katika baraza la usalama la umoja wa mataifa , baraza kuu la umoja wa mataifa limeahirisha kura hiyo hadi wiki ijayo ili kutoa nafasi kwa wanadiplomasia kutatua suala hilo.

Baraza hilo hadi sasa limefanya duru 35 za upigaji kura katika muda wa siku tatu, huku kura za kila nchi zikiwa hazionyeshi hatua yoyote ya ushindi.

Upigaji kura utaendelea hadi nchi moja itakapochaguliwa kutumikia kipindi cha miaka miwili kuanzia Januari mosi mwaka ujao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com