1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa mataifa, New York. Katibu mkuu kuanza ziara ya kwanza.

21 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZE

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon ataanza siku ya Jumanne ziara yake ya kwanza tangu kuchukua wadhifa huo wiki tatu zilizopita, kuhudhuria mkutano mjini Paris unaohusu ujenzi mpya wa Lebanon na mkutano wa umoja wa Afrika utakaohusisha zaidi suala la Darfur na Somalia.

Ziara ya kwanza ya Ban siku ya Jumatano itamfikisha hadi mjini Brussels , ambako atakuwa na mazungumzo tofauti na mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya Javier Solana , rais wa halmashauri ya Ulaya Jose Manuel Barroso na rais mpya wa bunge la Ulaya , Hans-Gert Pottering.

Katika mji mkuu wa Ubelgiji , Ban pia atakuwa na mazungumzo na mfalme Albert 11 kabla ya kukutana na waziri mkuu Guy Verhofstadt na waziri wa mambo ya kigeni wa Ubelgiji Karel De Gucht. Huenda pia akakutana na katibu mkuu wa NATO Jenerali Jaap de Hoop Scheffer.