Uhuru wa Waandishi wa habari nchini Rwanda
20 Oktoba 2009Matangazo
Huko Rwanda wakuu wanadhibiti zaidi habari kabla ya kufanyika uchaguzi wa mwakani, kwa muda wamesimamisha shughuli za vyombo vya habari vya kienyeji na vya kimataifa, na kufunga waandishi wa habari.
Rwanda imewekwa nambari ya 157 katika orodha ya nchi zinazokosolewa na Jumuiya ya Kimataifa ya waandishi wa Habari wasiojali mipaka.
Nimetafuta ukweli juuya hali ya waandishi wa habari huko Rwanda kwa kumpigia simu punde hivi Kayumba Casmir, mhariri wa hazeti la UKURI, yaani Ukweli, la huko Kigali. Madai hayo ya Jumuiya ya waandishi wa habari wasiojali mipaka yana ukweli kuhusu Rwanda?