1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Uhuru Kenyatta

Uhuru Muigai Kenyatta ndiye rais wa nne wa Jamhuri ya Kenya. Alichaguliwa mwaka 2013 na kurithi mikoba ya Mwai Kibaki. Ni mtoto wa Jomo Kenyatta, rais wa kwanza wa Kenya, na alimzaa na mke wake wa nne Ngina Kenyatta.

Uhuru Kenyatta alichaguliwa kuwa rais wa Kenya chini ya chama cha "The National Alliance" TNA, ambacho kilikuwa sehemu ya muungano wa Jubilee na chama cha mgombea mwenza wake William Ruto - cha "United Republican Party". Jina lake la Uhuru linatokana na neno la Kiswahili la uhuru na alipewa kutokana na matarajio ya uhuru wa Kenya uliyokuwa unategemewa. Desemba 15, 2010 Kenyatta alitajwa kuwa mshukiwa wa uhalifu dhidi ya ubinaadamu na mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC, kwa kupanga na kufadhili vurugu katika maeneo ya Naivasha na Nakuru. Hii ilikuwa inahusiana na vurugu zilizofuatia uchaguzi mkuu wa mwaka 2007/2008. Oktoba 2014 Mwendesha Mashtaka mkuu wa ICC Fatou Bensouda aliondoa mashktaka dhidi ya Kenyatta, akisema serikali ya Kenya ilikataa kutoa ushirkiano na hivyo hawakuwa na ushahidi w akutosha kundelea na kesi hiyo. Kenya aliwasilisha hoja katika Umoja wa Afrika kutaka mataifa ya umoja huo yajitoe katika ICC jumla - hoja ambayo iliungwa mkono na umoja huo.

Onesha makala zaidi