1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiKenya

ICC yasitisha uchunguzi machafuko baada ya uchaguzi Kenya

28 Novemba 2023

ICC yasitisha uchunguzi wa muda mrefu kuhusu machafuko ya baada ya uchaguzi wa Kenya ya 2007.

https://p.dw.com/p/4ZWjb
Uholanzi | Makao Makuu ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC
Makao Makuu ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICCPicha: Klaus Rainer Krieger/reportandum/IMAGO

Ofisi ya mwendesha mashataka wa Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu wa kivita.

ICC imetangaza kusimamisha uchunguziwake wa muda mrefu kuhusu machafuko yaliyosababisha umwagaji damu nchini Kenya yaliyozuka baada ya uchaguzi wa rais mwaka 2007. 

Uamuzi huo waICC umetangazwa katika wakati ambapo ofisi ya mwendesha mashataka wake ikitoa mwito wa kuomba   fedha za ziada kusimamia uchunguzi wa migogoro inayoendelea ikiwemo, Ukraine na vita vya Israel na Hamas. 

Uchunguzi ulioanzishwa mwaka 2010 kuhusu machafuko ya Kenya, ulifanikisha hatua ya kufunguliwa mashtaka watuhumiwa sita wakiwemo rais wa sasa na wa zamani wa nchi hiyo.

Soma pia:ICC yaongeza juhudi za kufufua kesi dhidi ya Joseph Kony

Ingawa  mahakama hiyo ilishindwa kuwatia hatiani kutokana na madai ya kutishwa kwa mashahidi pamoja na uingiliaji wa kisiasa.

Na baadae mashtaka yote dhidi ya watuhumiwa yalitupiliwa mbali. 
 

Wahanga wa maovu ya LRA wazungumzia masaibu yao