Ugonjwa wa kipundupindu wazuka Tanzania | Matukio ya Afrika | DW | 08.12.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Ugonjwa wa kipundupindu wazuka Tanzania

Watu wanne wamefariki dunia kutokanana ugonjwa wa kipindupindu katika mkoa wa Morogoro, nchini Tanzania

Watu wanne wamekufa na wengine 58 wamelazwa kufuatia mripuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika mkoa wa Morogoro mashariki mwa Tanzania.

Afisa wa Afya wa mkoa huo wa Morogoro Cares Lyimo ameliambia Shirika la habari la Ufaransa afp, kuwa kati ya watu hao wanne waliokufa watatu ni wa familia moja. Amesema mgonjwa wa kwanza aligundulika kuwa maradhi hayo wiki mbili zilizopita na kwamba mpaka sasa watu 58 wamelazwa kutokana na maradhi hayo ya kipindupindu.

Zaidi ya watu 60 walikufa kutokana na maradhi hayo mwezi Septemba na Oktoba mwaka huu katika mkoa wa Tanga uliyoko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.