Uchumi wa Dunia na kupanda kwa bei za vyakula ni mada za kutawala mkutano wa G8 leo | Habari za Ulimwengu | DW | 07.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Uchumi wa Dunia na kupanda kwa bei za vyakula ni mada za kutawala mkutano wa G8 leo

-

TOYAKO

Viongozi wa kundi la nchi nane tajiri kiviwanda duniani la G8 wanajiandaa kuanza mkutano wao wa siku tatu nchini Japan ambapo masuala muhimu yanayotazamiwa kuugubika mkutano huo ni pamoja na suala la uchumi wa dunia na kupanda kwa bei za vyakula pamoja na mafuta na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mkutano huo pia utahudhuriwa na viongozi wa China,India,Brazil na Afrika Kusini miongoni mwa wengine.Viongozi wa Afrika wanaohudhuria mkutano huo wanatazamiwa kuzungumzia wasiwasi wao juu ya kuzidi kupanda kwa gharaza za maisha hali ambayo imeongeza matatizo kwa watu maskini wa bara hilo.Aidha suala la Zimbabwe litajadiliwa ambapo viongozi wa G8 wanatazamiwa kulaani kwa pamoja kurudi tena madarakani kwa rais Robert Mugabe.Hali ya usalama imeimarishwa katika kisiwa cha kaskazini mwa Japan cha Hokkaido kwenye mji wa Toyako ambako mkutano huo unafanyika. Jana mamia ya waandamaji walijitokeza katika barabara za mji wa Sapporo ulioko karibu na eneo la mkutano kuwashinikiza viongozi wa G8 kuchukua hatua juu ya mabadiliko ya hali ya hewa,umasikini na kupanda kwa bei za vyakula duniani.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com