Uchumi wa China wagusa katika kila sehemu ya soko la dunia | Matukio ya Kisiasa | DW | 05.08.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Uchumi wa China wagusa katika kila sehemu ya soko la dunia

Jumatatu iliyopita kampuni la kuunda magari nchini China Geely imechukua umiliki wa kampuni la Sweden la kuunda magari la Volvo. Kampuni hilo limetoa kiasi cha dola bilioni 1,5.

default

Mfanyakazi akisafisha nembo ya moja ya mapampuni makubwa ya kuunda magari nchini China, kampuni la Volkswagen la Ujerumani mjini Shanghai.

Jumatatu iliyopita tarehe 02.08 kampuni la kuunda magari nchini China Geely litakuwa mmiliki wa kampuni la Sweden la kuunda magari la Volvo. Kiasi cha dola bilioni 1.5zimelipwa na kampuni hiyo ya China kwa kampuni hiyo ambaye hadi hivi karibuni ilikuwa ikimilikiwa na kampuni la Marekani la Ford. Mahusiano hayo ya Volvo ni uwekezaji wa hivi karibuni kabisa wa China wenye thamani ya mabilioni ya dola nchi za nje.

Baadhi ya nyakati ni muhimu kuangalia maendeleo katika mtazamo wa kihistoria. Ni karibu karne mbili - tangu 1820 , wakati ukoo wa kifalme wa Qing ulipokuwa ukiogelea katika mafanikio makubwa - ambapo udanganyifu katika utengenezaji wa bidhaa kutoka China unaharibu uchumi wa mataifa ya nchi zilizoendelea kiviwanda, kwa zaidi ya asilimia 30. 1978 kabla ya kuanza mageuzi, na sera za kufungua milango ya biashara hali ilikuwa ni asilimia 5 tu.

Katika wakati huo China ilikuwa inaonekana kuwa katika mwelekeo mzuri, wa kukamata tena nafasi yake kama soko kuu la kiuchumi . Katika miongo mitatu iliyopita dunia imeshuhudia mbio za kiuchumi za China ambazo hazina mfano wake, kwa wastani wa ukuaji wa uchumi wa kila mwaka nchini China wa asilimia kumi. China imejiweka mbele katika nafasi ya nchi ya kwanza duniani kusafirisha bidhaa nje. Katika biashara yake na nchi za nje, China ina wastani mkubwa kabisa, pekee katika mwaka uliopita imejipatia kiasi cha dola bilioni 200. Hifadhi ya fedha za kigeni ilizonazo kwa mujibu wa benki kuu ya nchi hiyo , Bank Of China, mwishoni mwa mwezi Julai imeongezeka kwa kiasi cha dola bilioni 2.4.

Pia kuna kiwango kikubwa cha sehemu ya hifadhi ya dhamana za serikali , hususan serikali ya Marekani. Lakini China inatumia hifadhi hiyo ya fedha za kigeni kwa werevu kwa kujiimarisha nafasi yake duniani. Karibu dola bilioni 50 zimetumiwa na makampuni ya China mwaka 2009 katika kuwekeza nchi za nje. Mzozo wa kiuchumi duniani umefanya uwekezaji huo kuwa ni kutafuta kununua kwa rahisi, katika kununua hususan makampuni kwa bei ya chini ambapo thamani yake itakuwa juu baadaye. Kwa hakika jicho la wafanyabiashara wa China linatua katika kuhakikisha upatikanaji wa mali ghafi katika ukuaji wa uchumi.

Juu kabisa katika orodha ya bidhaa za kununua ni zile zinazohusiana na mafuta na gesi pamoja na makampuni makubwa ya ujenzi.

China inaonekana kuwa yenye ubunifu mkubwa katika mipango yake ya uwekezaji katika nchi zinazoendelea. Katika bara la Afrika unafanyika mpango wa ujenzi wa miundo mbinu kwa kupata malighafi. China inajenga barabara , reli na inapata madini ya chuma , shaba pamoja na mafuta. Na kutokana na hali hiyo China imeongeza uwekezaji katika sekta ya mali ya asili barani Afrika kwa asilimia 75.

Wakati huo huo China inatumia lengo lake la uwekezaji kuweza kuongeza zaidi ukuaji wa uchumi wake. China haitosheki kabisa, kiwanda hicho cha dunia, kinazalisha pia bidhaa kwa ajili ya mataifa ya magharibi. Pia inataka China kuuza bidhaa zake katika soko la dunia. Kwa upande wa bidhaa rahisi China inaongoza pia katika kila sehemu. Lakini katika viwango vya bidhaa za thamani ya juu na zenye ubora wa hali ya juu, bado mataifa ya magharibi yanaongoza.

Mwandishi : von Hein, Matthias / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri: Mohammed Abdul Rahman.

 • Tarehe 05.08.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Od4o
 • Tarehe 05.08.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Od4o
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com