TOLOUSE: Wafanyakazi wa Airbus waandamana | Habari za Ulimwengu | DW | 06.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TOLOUSE: Wafanyakazi wa Airbus waandamana

Maelfu ya wafanyakazi katika viwanda vinne vya kampuni ya ndege ya Airbus nchini Ufaransa wamefanya mgomo wa siku moja hii leo kupinga mpango wa kampuni hiyo kupunguza nafasi 10,000 za ajira.

Kwa mujibu wa mpango wa kuifanyia mageuzi kampuni ya Airbus, uliotangazwa wiki iliyopita, zaidi ya nafasi 4,000 za ajira zitapunguzwa nchini Ufaransa. Kampuni ya EADS iliyoibuni kampuni ya Airbus, imesema inahitaji kupunguza matumizi kwa kiasi cha yuro bilioni tano kuinusuru kampuni ya Airbus baada ya kucheleweshwa kwa utengenezaji wa ndege aina ya Airbus 380.

Kansela wa Ujerumani, Bi Angela Merkel, na mgombea urais wa Ufaransa, Segolene Royal, wameujadili mpango wa Airbus hii leo mjini Berlin.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com