Tanzania: Sakata la Dowans | Matukio ya Kisiasa | DW | 29.09.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Tanzania: Sakata la Dowans

Nchini Tanzania Mahakama Kuu ilitoa hukumu ya kuridhia malipo ya fidia ya fedha kwa Kampuni ya ya Dowans ambayo ilisajili,tuzo yake iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC).

default

Watanzania wakabiliwa na mgao wa umeme

Kufuatia uamuzi huo Shirika la umeme TanzaniaTanesco sasa linatakiwa iilipe Dowans kiasi cha Sh111 bilioni, badala ya Shilingi 94 bilioni za awali ikiwa ni pamoja na riba ya asilimia 7.5.
Aboubakary Liongo alizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, amesema hukumu hiyo ni matokeo ya wanasiasa kutofuata ushauri wa kitaalam na kuweka mbele maslahi ya kisiasa.

Mwandishi:Aboubakary Liongo

Mhariri:Othman Miraji

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com