Tanzania: Nani atakuwa mtetezi wa CCM kwa urais wa Zanzibar? | Matukio ya Kisiasa | DW | 08.07.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Tanzania: Nani atakuwa mtetezi wa CCM kwa urais wa Zanzibar?

Shein, Bilal, Nahodha au Shamhuna, mtetezi wa CCM kwa urais wa Zanzibar?

Wakati huo huo, washabiki wa watetezi wanaowania kupata kibali cha uongozi wa chama tawala cha CMM kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu wamefika mjini Dodoma kuwapigia debe watu wanaowaona wanafaa kukamata nafasi hiyo. Watu wanaotajwa na kuzungumziwa sana kuwa huenda wakachomoza kushinda, kati ya majina 11 yaliowasilishwa kwa kamati kuu ya chama cha CCM, ni Dr. Ali Shein, makamo wa sasa wa rais wa Jamhuri ya Muungano; Dr. Gharib Bilal, aliywahi kuwa waziri kiongozi wa Zanzibar; waziri kiongozi wa sasa wa Zanzibar, Shamsu Vuai Nahodha; na naibu wa waziri kiongozi wa sasa wa Visiwani Zanzibar, Ali Juma Shamhuna.

Othman Miraji alizungumza punde hivi na mmoja wa makada wa CCM kutoka Zanzibar waliofika Dodoma kushawishi wajumbe wa Halmashauri kuu ya taifa wamuunge mkono mtu wao: Naye ni Bakari Shamte...

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

 • Tarehe 08.07.2010
 • Mwandishi Samia Othman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OEFN
 • Tarehe 08.07.2010
 • Mwandishi Samia Othman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OEFN

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com