1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Jakaya Kikwete

Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa rais wa nne wa Tanzania, akikaa madarakani kuanzia 2005 hadi 2015. Kabla ya kuchaguliwa kwake, alikuwa waziri wa mambo ya nje kuanzia 1995 hadi 2005 chini ya mtangulizi wake Benjamin Mkapa.

Kikwete alizaliwa Oktoba 7, 1950. Kati ya 1959 na 1963, alisomea katika shule ya msingi Karatu nchini Tanzania, kabla ya kujiunga na shule ya kati Tengeru kaunzia 1962 hadi 1965. Baada ya Tengeru alihamia shule ya sekondari Kibaha kwa masomo yake ya sekondari kati ya 1966 hadi 1969, na alijiunga na shule ya Tanga kwa masomo ya cheti cha juu cha sekondari. Alihitimu katika chuo kikuu cha Dar es Salama 1975 na shahada ya uchumi. Kama kada wa chama cha Mapinduzi, Kikwete alitoka kwenye ngazi moja hadi nyengine katika ujenzi wa chama, hadi alipofikia ngazi ya mwenyekiti wa taifa wa chama hicho kikongwe barani Afrika.

Onesha makala zaidi