Tanzania: Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima afikishwa Mahakamani
21 Desemba 2011Matangazo
Swali hapa ni je Kwa upande mmoja au mwengine wanahabari wanawajibika katika kutekeleza wajibu wao? Ama ni uonevu tu na ukandamizaji wa vyombo vya habari?
Nchini Tanzania mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda, jana alifikishwa mahakamani kwa kupitisha makala inayowashawishi askari na maafisa wa jeshi nchini Tanzania kuacha kuitii Serikali.
Kufahamu mengi juu ya hilo Amina Abubakar amezungumza na Bw. Kajubi Mokajanga katibu mtendaji wa chama cha wanahabari nchini Tanzania.
Mwandishi Amina Abubakar
Mhariri Mohammed Abdulrahman