TAMIL TIGERS:Waushambulia kwa mabomu uwanja wa ndege wa Sri Lanka | Habari za Ulimwengu | DW | 26.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TAMIL TIGERS:Waushambulia kwa mabomu uwanja wa ndege wa Sri Lanka

Waasi wa Tamil Tigers, wamekishambulia kwa mabomu kituo cha jeshi la anga la Sri Lanka, kilichoko katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa nchi hiyo, kaskazini mwa mji mkuu Colombo ambapo wananga wawili wameuawa na wengine 17 kujeruhiwa.

Msemaji wa waasi hao wa Tamil Tigers ametahadharisha kuwa mashambulizi zaidi yatafuatia.

Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Sri Lanka umefungwa kwa muda kwa tahadhari ya mashambulizi zaidi.

Waasi wa Tamili Tigers mnamo mwezi Julai mwaka 2001 walikishambulia kituo hicho hicho, na kuwaua watu 18 pamoja na kuharibu ndege za kijeshi na za abiria zilizokuwepo.

Makubaliano ya kusitisha vita kati ya waasi na serikali yametupiliwa mbali na pande zote mbili kwa miezi kadhaa sasa, na wadadisi wanasema kuwa nchi hiyo inarejea tena katika vita vya wenyewe kwa wenyewe,

Zaidi ya watu elfu 4 wameuawa katika miezi 15 iliyopita kutokana na mzozo kati ya pande hizo mbili.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com