Talabani awataka wanajeshi wa Marekani wamuachilie huru haraka afisa wa Iran | Habari za Ulimwengu | DW | 23.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Talabani awataka wanajeshi wa Marekani wamuachilie huru haraka afisa wa Iran

Baghdad:

Rais Jalal Talabani wa Iraq ametoa mwito afisa wa Iran anaeshikiliwa na wanajeshi wa Marekani katika eneo la wakurd kaskazini mwa Iraq,aachiwe huru haraka.Jalal Talabani amesema vikosi vya Marekani vimeudhalilisha utawala wa wakurd kwa kupuuza sheria zao na kutowasiliana nao walipomkamata muakilishi wa walinzi wa mapinduzi ya Iran.Afisa huyo wa ngazi ya juu wa Iran anatuhumiwa na vikosi vya Marekani kuhusika na biashara haramu ya miripuko.Pande zote mbili,serikali ya mjini Baghdad na viongozi wa serikali ya Iran wanasisitiza afisa huyo,alikua katika ziara ya serikali nchini Iraq kutokana na mwaliko wa viongozi wa utawala wa ndani wa wakurd.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com