1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Takataka za sumu mjini Abidjan zapelekwa Le Havre Ufaransa

28 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCyV

Abidjan:

Meli ya Ufaransa imeng’owa nanga toka bandari ya Abidjan ikiwa na shehena ya kwanza ya takataka za sumu zilizomwaga kwa siri nchini Cote d’Ivoire.Meli hiyo inatazamiwa kuwasili katika bandari ya Le Havre siku kumi kutoka sasa..Tangu mwezi mmoja uliopita kampuni moja la kuzowa takataka la Ufaransa limekua likichimba mabaki ya mafuta ya sumu.Kampuni la Uholanzi linalaumiwa kuhusika na kumwagwa Agosti iliyopita takataka za sumu nje ya mji mkuu wa kibiashara wa Cote d’Ivoire-Abidjan.Takataka hizo zimegharimu maisha ya watu kumi na wengine zaidi ya laki moja kulazimika kupatiwa matibabu.Watu sabaa wamekamatwa,wakiwemo watumishi wawili wa kampuni la Uholanzi.