1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SUVA: Kiongozi wa kijeshi nchini Fiji aapishwa kuwa waziri mkuu wa muda.

5 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdB
Dr..Rice amlahki Bw.Steinmier huko Berlin
Dr..Rice amlahki Bw.Steinmier huko BerlinPicha: AP

Kiongozi wa mapinduzi ya Fiji, Frank Bainimarama, ameapishwa kuwa waziri mkuu wa muda wa nchi hiyo.

Hayo yanatokea mwezi mmoja tangu kiongozi huyo alipoongoza mapinduzi dhidi ya serikali ya Waziri mkuu, Laisenia Qarase, iliyochaguliwa na umma.

Frank Bainimarama ametangaza ataendelea kushikilia wadhifa wa mkuu wa majeshi na kwamba wanajeshi waliohusika na mapinduzi watapewa kinga kutokana na jukumu lao kwenye mapinduzi.

Frank Bainimarama hakutangaza wakati taifa hilo linapotarajiwa kuandaa uchaguzi.

Majeshi ya Fiji yameshutumiwa vikali na jumuiya ya kimataifa huku baadhi ya nchi zikiiwekea vikwazo Fiji.