Spian katika Qasri la mfalme: | Michezo | DW | 01.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Spian katika Qasri la mfalme:

Spain, mabingwa wapya wa Ulaya,walipokewa leo rasmi na mfalme na malkia.

Spian,mabingwa wapya wa Ulaya walipokewa rasmi jana na mfalme Juan carlos na Malkia Sofia katika Qasri lake .Baadae waziri mkuu Jose Luis Zapatero akawatembelea wachezaji.

Kocha wa makamo-bingwa Ujerumani Joachim Loew,anasema hapangi mageuzi makubwa ya timu yake kabla kombe la dunia 2010 Afrika kusini.Na Msumbiji imegonga kengele ya hatari kuwa biashara imeongezeka ya kuwasafirisha wasichana wa Msumbiji kufanya kazi za umalaya Afrika kusini kabla kombe la dunia 2010.

►◄

Kocha wa Spian,mabingwa wa Ulaya walioilaza juzi Ujerumani bao 1:0- mzee Luis Aragones aliandamana jana na timu yake hadi Qasri la kifalme la Zarzuela akibeba kombe la Ulaya .Wakapokewa rasmi na mfalme Juan Carlos na malkia Sofia.Baadae timu hiyo ikamtembelea waziri mkuu Zapatero aliekuwapo pia uwanjani mjini Vienna,juzi jumapili wakati wa finali ya kombe la Ulaya.

Sehemu kubwa ya mashabiki wa Spian wanamtaka mzee Aragones aliewapatia kombe baada ya kiu cha miaka 44 asalie kitini kama kocha wa Spina.Aragones, akiwa na umri wa miaka 70 Julai hii,hakupendwa sana katika kipindi chake cha miaka 4.

Nae kocha mwenzake wa Ujerumani, Joachim Loew,amearifu jana kwamba hapangi mabadiliko makubwa katika kikosi chake kinachojiwinda kwa kombe la dunia 2010.

Loew alisema,

"Ni wazi kwamba tutaingiza wachezaji wapya,lakini timu haitabdilishwa mno."-alisema Loew. Akasema zaidi kwamba, nahodha Michael ballack na stadi wa kiungo mwenzake Torston Frings wote wakiwa na umri wa miaka 31 hivi sasa bado wana uchu wa kujipatia ushindi.

Akasema kipa mwenye umri wa miaka 38 Jens Lehmann bado hakutangaza kustaafu katika timu ya taifa.

Mwenzake Oliver Kahn alistaafu mara tu kumalizika kwa kombe lililopita la dunia.

Mchezaji alieichezea sana timu ya taifa ya Ujerumani kuliko yeyote mwengine, Lothar Matthaeus ,aliwasili leo mjini Tel Aviv ili kuwa kocha wa klabu ya Maccabi Netanya. Akiwa na umri wa miaka 47, ataanza kesho kuifunza timu hiyo ya ligi ya Israel baada ya kufunga mkataba wa miaka 2.Maththaeus ameichezea Ujerumani mara 150 na ameibuka mara 7 mabingwa na bayern munich katika Bundesliga.

Rais wa UEFA-shirikisho la dimba la Ulaya ,mfaransa Michel Platini,amemungamkono kocha wa timu ya Ufaransa Raymond Domenech kubakia kocha wa taifa licha ya msiba ulioikumba Ufaransa katoka kombe la Ulaya 2008.

Taarifa kutoka Maputo,zinasema polisi nchini msumbiji ilionya jana kuwa misafara inaongezeka ya kuwapelerka wasichana wadogo wa msumbiji Afrika kusini kwa biashara ya umalaya katika kipindi hiki kinachotangulia kombe la dunia 2010.

Polisi imearifu kuna magengi yanayotumia kombe lijalo la dunia Afrika kusini ,kuwasafirisha wasichana wa kati ya umri wa miaka 13 na 18 kwa kuwaahidi maisha bora huko Afrika kusini kutokana na kuongezeka kwa raslimali zaidi.

Visa vingi vya safari hizo vimegunduliwa miezi ya karibuni.Hadi wageni 450,000 wanatarajiwa kuhudhuria kombe la dunia 2010,Afrika kusini ikiwa nchi ya kwanza kuliandaa barani Afrika.

Bingwa mtetezi wa mashindano ya tennis ya Wimbledon

muamerika Venus Williams ameingia jana nusu-finali baada ya kumtimua nje Tamarine Tanasugarn.Bingwa huyo mara 4 atakumbana sasa ama na Elena Dementieva au nadia Petrova.Alishinda kwa setu 2- 6-4 na 6-3.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com