Spain ni mabingwa wapya wa Ulaya | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 30.06.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

IDHAA YA KISWAHILI

Spain ni mabingwa wapya wa Ulaya

Spain jana iliizaba Ujerumani bao 1:0 na kutawazwa mabingwa baada ya miaka 44.

Spain ikimtia munda Ballack

Spain ikimtia munda Ballack

Kombe la Ulaya 2008 limemalizika kwa Spain kukata jana usiku kiu cha miaka 44 tangu ilipotawazwa mara ya mwisho na pekee, mabingwa wa Ulaya.Spain ni mabingwa wapya wa Ulaya baada ya kuikomea Ujerumani bao 1:0 na Ujerumani -mabingwa mara 3 wameibuka makamo-bingwa mjini Vienna.

Timu ya Ujerumani itawasili ingawa bila ya kombe adhuhuri hii mjini Berlin na mashabiki wake maalfu kadhaa watasipokea kwa sha ngwe na shamra shamra na nje ya lango kuu la Brandenburg.

►Kombe la ulaya 2008 litaingia katika historia ndilo lililosisimua mno kuliko yote hadi sasa kwa kile kilichopita tangu viwanjani na hata angani katika miji ya nchi mbili zilizoandaa kombe hili kwa ubia-Austria na Uswisi.

Jumla ya mechi 31 zilichezwa na magoli 77 yalitiwa kimiyani.Tulijionea mechi nyingi za kushambulia-attacking gamrs-,magoli ya kusisimua ya dakika za mwisho na shangwe na shamra shamra mitaani miongoni mwa mashabiki-kuanzia Juni 7 hadi 29,mada kuu Ulaya nzima ilikua kombe la Ulaya, la pili kwa ukali na msisimko baada ya kombe la dunia la FIFA.

Nusu-finali zote mbili jumatano na alhamisi iliopita zilisisimua ajabu-tulijonea mechi sio za kujilinda na zilizotoa mshindi baada ya dakia ya 90 ya mchjezo kama lile bao la Philipp Lahm katika lango la Uturuki.

Bila ya shaka tulijionea nyakati za jazba na patashika katika finali ya jana na hasa pale David Silva na Lukas Podolski walipokaribia kupigana vichwa ingawa si kwa kipimo kile cha finali ya kombe la dunia kati ya Zinedine Zedane na Materrazi.

Ni wachezaji 3 waliotolewa nje ya uwanja katika mechi 31,lakini si kadi hata moja nyekundu ilitolewa kwa mchezo mbaya sana wa ngware.

Kushindwa duru ya kwanza tu kwa timu 2 wenyeji-Austria na Uswisi, kulitarajiwa hatahivyo, kupigwa kwao kumbo nje ya mashindano na mapema hakujalemaza mashindano kama ilivyokua Ghana katika kombe la Afrika baada ya Black Stars kutolewa-nusu-finali.

Mashabiki wa Ujerumani,Croatia,Uturuki na waspain waliowasili Austria na Uswisi, si mbali na mpaka wa nchi zao walichangia sana kumpunga shetani wa dimba:

Na Spian ilipoilaza jana Ujerumani bao 1:0-bao la Torres,mashabiki wa Ujerumani hawakuangua kilio au kuzusha fujo. Baadhi yao walisema hivi:

"Wajerumani wamecheza vibaya-waspian wamecheza uzuri."

Shabiki mwengine kati ya maalfu kadhaa watakaoikaribisha timu ya Ujerumani-makamo-bingwa mjini Berlin,alaasiri ya leo, alisema:

"Ah, hatukuvunjika moyo,tumetokea wapili na hii simbaya-hatusikitiki-kwani mara ijayo tuitashinda."

Na nini amesema kocha wa Ujerumani Joachim Loew baada ya pigo la jana :

."Inatubi leo kuzitanbua sifa bora za dimba la waspain.Wamecheza maridadi ajabu na hasa kiufundi walitamba kweli."

Na nahodha wa Ujerumani Michael Ballack.ambae kwa mara nyengine tena jahazi lake limeenda mrama asemaje ?

"Pumzi zetu hazikutosha na mashindano yalikua marefu.Tulitaka sana kushinda,lakini hatukuweza kucheza barabara."

Mbali na hali ya hewa iliokatiza matangazo Ujerumani ilipocheza na Uturuki huko Basel-jambo ambalo lilipindukia mamlaka ya UEFA kulizuwia,kombe la Ulaya limeenda uzuri.

Sasa kuna kila sababu kuzidi kupanuliwa kutoka timu 16-24.

Halmashauri Tendaji ya UEFA itazungumzia swali hilo katika kikao chake Septemba mwaka huu ,itakapoamua iwapo kombe lijalo lichezwe kama ilivyopangwa 2012 Ukraine na Poland au la.Sasa macho ya mashabiki yanakodolewa mashindano makuu yajayo-wiki 6 kutoka sasa-michezo ya Olimpik ya Beijing.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com