Sherehe za tamasha la muziki wa Bayreuth kuanza Jumapili | Habari za Ulimwengu | DW | 23.07.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Sherehe za tamasha la muziki wa Bayreuth kuanza Jumapili

Pazia litafunguliwa mwishoni mwa juma hili katika tamasha la muziki la Bayreuth hapa Ujerumani, ambalo linatarajiwa kufunguliwa rasmi kwa muziki mpya wa opera wa Richard Wagner.

Kiongozi wa muda mrefu wa tamasha la muziki la Bayreuther Festspiele, Wolfgang Wagner, akiwa mbele ya jengo la ukumbi wa Bayreuth , wa Festspielhaus.

Kiongozi wa muda mrefu wa tamasha la muziki la Bayreuther Festspiele, Wolfgang Wagner, akiwa mbele ya jengo la ukumbi wa Bayreuth , wa Festspielhaus.

Pazia litafunguliwa mwishoni mwa juma hili katika tamasha la kale nchini Ujerumani la Bayreuth, ambalo linatarajiwa kufunguliwa rasmi kwa muziki mpya wa opera wa Richard Wagner unaofahamika kama Lohengrin.

Julai 25 , siku ya Jumapili linaanza tamasha la 99 la Bayreuther, tamasha la kila mwaka majira haya ya kiangazi. tamasha la muziki ambalo linalenga tu katika kazi za Wagner na litakuwa la kwanza tangu kifo cha mjukuu wa mtunzi huyo maarufu ambaye alikuwa mkuu wa zamani wa tamasha hilo, Wolfgang Wagner, mapema mwaka huu.

Kuchezwa kwa muziki huo mpya unaojuliakana kama Lohengrin kunakosubiriwa kwa shauku kubwa , kunakotarajiwa kufanywa na muongozaji maarufu nchini Ujerumani Hans Neuenfels, mwenye umri wa miaka 69, ni tayarisho jipya ambalo litaonyeshwa katika ukumbi wa Festspiehaus mjini Bayreuth katika muda wa miaka miwili.

Tamasha la mwaka jana lilikuwa tu la kumbukumbu ya ngano za zamani katika muziki na kuruhusu mabadiliko ya uongozi katika ngazi ya juu kwa njia isiyo na utata. Wagner ambaye alitawala katika vilima vya Green Hill huko Bayreuth kwa mkono wa chuma kwa miaka 57 alikabidhi u hatamu za uongozi kwa wanawe wa kike, Eva Wagner-Pasquier, mwenye umri wa miaka 65 na Katharina Wagner mwenye umri wa miaka 32.

Kwa hiyo , Lohengrin , utakuwa utayarishaji mpya wa kwanza chini ya uongozi mpya wa pamoja kama anavyoelezea Christian Thielemann ambaye ni mmoja wa waongozaji katika tamasha la Bareuth.

Tunaangalia kwa undani muziki huu wa Wagner, na hatuwezi kusahau, watu wa kwaya na wanamuziki kuwa wanakuja hapa kwa ajili ya mapumziko yao. Pia wanajumuika katika kupiga muziki kwa mapenzi yao. Yule anayekuja hapa, anataka kuja. Na hili ndio muhimu sana. Hakuna utaratibu wa kazi. Hapa tunapiga muziki, yule asiyetaka, halazimiki kuja hapa.

Kwa kuwa na nyota wa sauti ya tatu nyembamba kutoka hapa Ujerumani Jonas Kaufmann akiwa ndio kwanza anajitokeza katika tamasha hili la mjini Bayreuth , akiwa anachukua nafasi ya juu, pamoja na kijana anayekuja juu pia ambaye ni muongozaji kutoka Latvia Andris Nelsons , matarajio yako juu sana kuliko kawaida.

Bayreuth ni moja kati ya maeneo muhimu sana katika matamasha ya muziki wa opera pamoja na muziki laini, ambapo watu hutoa maombi ya kuingia katika tamasha hilo, ikiwa orodha inafika hadi miaka kumi. Tamasha hilo huanza kwa kawaida Julai 25 hadi August 28 na siku ya ufunguzi huhudhuriwa kwa kawaida na Wajerumani ambao ni maarufu kijamii na kisiasa.

Mwandishi : Sekione Kitojo / AFPE

Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman

 • Tarehe 23.07.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OTMq
 • Tarehe 23.07.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OTMq
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com