SHARM EL-SHEIKH: Israel kuachilia huru wafungwa 250 wa Fatah | Habari za Ulimwengu | DW | 26.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SHARM EL-SHEIKH: Israel kuachilia huru wafungwa 250 wa Fatah

Waziri Mkuu wa Israel,Ehud Olmert ametangaza mpango wa kuwaachilia huru wafungwa 250 wa chama cha Fatah cha Rais wa Wapalestina,Mahmoud Abbas. Olmert alitoa tangazo hilo mwishoni mwa mkutano wa kilele wa pande nne uliofanywa katika mji wa kitalii wa Sharm el-Sheikh nchini Misri.Mbali na Olmert na Abbas,mkutano huo ulihudhuriwa pia na Mfalme Abdallah wa Pili wa Jordan na mwenyeji Rais Hosni Mubarak wa Misri.Hadi Wapalestina 10,000 wapo katika jela za Israel.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com