Serikali ya Tanzania yamruka Makonda kuhusu mashoga | Matukio ya Afrika | DW | 05.11.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Serikali ya Tanzania yamruka Makonda kuhusu mashoga

Tanzania imesema mpango wa kuwasaka na kuwakamata watu wanaoshukiwa kuwa mashoga uliotangazwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam siyo sera rasmi, na kujitenga na mpango huo uliokosolewa na mashirika ya haki za binadamu.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na  mwenye nguvu na usemi kisiasa , Paul Makonda, aliwasihi wakazi wa mmkoa wake wiki iliyopita kuanza kuwaripoti mashoga ili waanze kukamatwa. Wizara ya mambo ya nje ya Tanzania imesema katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumapili kuwa "haya ni maoni binafsi ya Makonda na siyo msimamo wa serikali."

Iliongeza kuwa serikali itaendelea kuheshimu mikataba yote ya kimataifa kuhusu haki za binadamu ambayo iliiridhia. Makonda, mkristu mwenye hamasa na mshirika mtiifu kwa rais John Magufuli, alisema tabia za ushoga zinakwneda kinyume na maadili ya Watanzania na dini kuu mbili za Kikristu na Kiislamu.

Matamshi yake yalikosolewa na mashirika kadhaa yakiwemo Amnesty International na Umoja wa Mataifa. Chini ya sheria za wakati wa ukoloni wa Uingereza, ushoga ni kinyume cha sheria nchini Tanzania na ngono kati ya watu wa jinsia moja inaweza kuadhibiwa kwa kifungo cha hadi miaka 30 gerezani.

Tansania Daressalam Paul Makonda (DW/S. Khamis)

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania, Paul Makonda. Picha na Said Khamis.

Hisia za kuwachukia mashoga na Wasagaji ziliongezeka tangu Magufuli alipoingia madarakani mwaka 2015, na kuwalaazimu mashoga na wasagaji wengi kuishi kwa kujificha. Mwaka uliopita, rais alismea kila mtu anapaswa kulaani ushoga, "hata ng'ombe" na muda mfupi baadae serikali ilitishia kuwakamata na kuwafukuza watetezi wa haki za mashoga.

Raia wa tatu wa Afrika Kusini walitimuliwa kwa madai ya kutetea ndao za jinsia moja. Kliniki za matibabu ya ukimwi pia zimefungwa chini Magufuli, zikituhumiw akwa kuendeleza ushoga, huku rais huyo akiwaambia wanawake waachane na uzazi wa mpango na kuzaa watoto wengi.

Siku ya Jumamosi, Umoja wa Ulaya ulisema umemuita mwakilishi wake mkuu mjini Brussels kwa majadiliano, kufuatia ripoti kwamba aliombwa na serikali kuondoka. Brussels pian ilikosoa kile ilichokiona kama kuzidi kwa ukiukaji wa haki za binadamu nchini Tanzania.

"Umoja wa Ulaya unasikitika juu ya kuporomoka kwa haki za binadamu na utawala wa sheria nchini Tanzania na utafanya tathmini pana ya uhusiano wake na Tanzania," msemaji wake Sudanne Mbise alisema katika taarifa.

Siku ya Jumamosi, Marekani iliwashauri raia wake walioko Tanzania kupitia upya shughuli zao za kwenye mitandao ya kijamii na intaneti, na kuondoa mambo yoyote yanayoweza kukiuka sheria za Tanzania kuhusu vitendo vya ushoga.

Mwandishi: Iddi Ssessanga/afpe,rtre.

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman