1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz aonya kitisho cha kuimarika kwa chama cha AfD

Lilian Mtono
6 Septemba 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amekishambulia chama cha siasa kali za mrengo wa kulia AfD, akikifananisha na kikosi cha kuibomoa Ujerumani na kuonya kwamba sera zake zitaharibu ustawi wa nchi.

https://p.dw.com/p/4W0CH
Kansela Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz Picha: picture alliance

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amekishambulia chama cha siasa kali za mrengo wa kulia AfD, akikifananisha na kikosi cha kuibomoa Ujerumani, na kuonya kwamba sera za utaifa ambazo chama hicho kinapigania zitaharibu ustawi wa nchi.

Matamshi hayo makali ya Scholz dhidi ya chama hicho mbadala kwa Ujerumani yanatolewa wakati kikishuhudia kuongezeka kwa ushawishi wake nchini Ujerumani, wakati matokeo ya karibuni ya uchunguzi wa maoni yakionyesha kinabalika kwa asilimia 22, na kukipiku chama cha SPD cha kansela Scholz kilichopata asilimia 16.

Scholz aidha ameonya dhidi ya mwito wa AfD wa kurejea kwenye uzalendo akisema si chochote bali unalenga kuuvunja Umoja wa Ulaya na kubomoa kwa kiasi kikubwa ustawi wa Ujerumani.