RIGA: Vingozi wa nchi nane za umoja wa ulaya wakamilisha mkutano | Habari za Ulimwengu | DW | 11.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

RIGA: Vingozi wa nchi nane za umoja wa ulaya wakamilisha mkutano

Marais wanane wa nchi za umoja wa ulaya wamekamilisha mkutano wao katika mji mkuu wa Riga nchini Latvia.

Kikao hicho kilizingitia maswala ya mabadiliko ya hali ya hewa na kuhusu marekebisho ya katiba ya umoja wa ulaya.

Rais Heinz Fischer wa Austria amesisitiza makubaliano ya katiba ambayo yamekwama kuafikiwa tangu wapiga kura wa Ufaransa na Uholanzi kupinga katika kura ya maoni ya mwaka 2005.

Marais kutoka Austria, Finland Ujerumani, Hungary, Italia, Latvia, Poland na Portugal walihudhurila kikao hicho.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com