1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramallah. Israel yawaacha huru wafungwa wa Kipalestina.

21 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgi

Israel imewaacha huru wafungwa 255 wa Kipalestina ikiwa kama sehemu ya juhudi zinazoongozwa na Marekani za kuimarisha utawala wa rais Mahmoud Abbas na kukitenga chama hasimu cha Hamas katika eneo la Gaza.

Mamia ya ndugu waliokuwa wakifurahia pamoja na waliokuwa wakiunga mkono waliyalaki mabasi ambayo yalivuka katika kituo cha upekuzi cha Beituniya nje ya eneo la Ramallah katika ukingo wa magharibi.

Wengi wa wafungwa hao wanatoka katika chama cha Fatah cha rais Abbas, ambaye amewaita mashujaa wa uhuru. Ni pamoja na wanawake sita pamoja na Abdel Rahim Malouh ambaye ni kiongozi wa pili katika kundi dogo la tawi la chama cha PLO, Popular Front for the Liberation of Palestina, ambalo limehusika katika kifo cha waziri mmoja wa Israel mwaka 2001. Kwa jumla , Israel inawashikilia wafungwa 11,000 wa Kipalestina.