Rais wa Palestina ahutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 26.09.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Rais wa Palestina ahutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Katika hotuba yake, Rais huyo wa Palestina Mahmoud Abbas aliitaka Israel kuchagua kati ya amani au ujenzi wa makaazi katika Ukingo wa Magharibi.

Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas akipeana mkono na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.

Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas akipeana mkono na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.

Katika hotuba yake kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas amelaani kile alichokiita ''fikra za upanuzi na utawala'' za Israel.

Rais Abbas amesema Israel lazima ichague kati ya amani au ujenzi wa makaazi katika Ukingo wa Magharibi, kama inataka mafanikio katika mazungumzo ya amani ya kimataifa.

Muda wa kusimamisha ujenzi wa makaazi kwa kipindi cha miezi kumi katika Ukingo wa Magharibi unamalizika hii leo.

Rais Barack Obama wa Marekani na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani wamesema Israel lazima iongeze muda huo na iendelee na mazungumzo ya amani yaliyoanza upya mwanzoni mwa mwezi huu baada ya kukwama kwa karibu miaka miwili.

 • Tarehe 26.09.2010
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/PMrX
 • Tarehe 26.09.2010
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/PMrX
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com