Rais wa Chad ajitokeza hadharani | Habari za Ulimwengu | DW | 07.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Rais wa Chad ajitokeza hadharani

NDJAMENA:

Serikali ya Chad inasema,imedhibiti nchi baada ya kuvitimua vikosi vya waasi kutoka mji mkuu Ndjamena.Rais Idriss Deby akijitokeza hadharani kwa mara ya kwanza tangu waasi kuushambulia mji wa Ndjamena mwishoni mwa juma,amemlaumu rais wa nchi jirani Sudan,Omar Hassan al-Bashir kuwa aliwasaidia waasi hao.Lawama hiyo lakini imekanushwa na Rais wa Sudan.

Wakati huo huo,Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Herve´Morin katika ishara ya kuiunga mkono serikali ya Chad,aliwasili nchini humo bila ya ziara hiyo kutangazwa hapo kabla.Maafisa wa Msalaba Mwekundu nchini humo wanasema,mamia ya raia wameuawa na takriban 1,000 wengine wamejeruhiwa katika mapigano yaliyozuka baada ya vikosi vya waasi kushambulia majeshi ya serikali hapo siku ya Jumamosi katika jeribio la kutaka kumpindua Rais Deby.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com