Rais wa ANC Zuma | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 22.04.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Rais wa ANC Zuma

Rais wa chama kinachotawala nchini Afrika Kusini ANC Jacob Zuma ataka viongozi wa Afrika waingilie kati Zimbabwe.

default

Rais wa chama kinachotawala nchini Afrika Kusini ANC Jacob Zuma .


►◄


Rais wa chama kinachotawala nchini Afrika Kusini ANC Jacob Zuma amesema  kucheleweshwa  kutolewa matokeo ya uchaguzi nchini Zimbabwe ni jambo lisilokubalika  na  amewata viongozi  wa Afrika wachukue hatua ili kusuluhisha katika mgogoro wa nchi hiyo.

Bwana Zuma  amesema hayo leo mjini Berlin katika ziara yake fupi nchini Ujerumani.

Akizungumza katika mahojiano  kiongozi huyo wa chama cha ANC amesema kuchelewesha kutoa matokeo ya uchaguzi  hakuwasaidii watu wa Zimbabwe. 

Watu wa Zimbabwe walipiga kura tareha 29  mwezi machi kulichagua bunge  na rais, lakini matokeo ya uchaguzi huo bado hayajatangazwa hadi leo.  Na hata zoezi la kuhesabu tena  kura pia limecheleweshwa.Kutokana na hayo amewataka viongozi wa  Afrika wachukue  hatua ili wasuluhishe  katika mgogoro wa Zimbabwe.

Amesema  Afrika  inapaswa  kuchagua wajumbe watakaoenda  Zimbabwe na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa pande  zote  ikiwa pamoja  na wajumbe wa tume ya uchaguzi.

Katika ziara yake nchini Ujerumani kiongozi huyo wa chama cha ANC Jacob  Zuma alikutana na bwana  Kurt Beck mwenyekiti wa chama cha Social Demokratik kilichomo katika serikali ya mseto ya Ujerumani.  Zuma  anaefanya ziara ya nchi  kadhaa  za Ulaya anatarajiwa  kufanya  mazungumzo  na waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown  kesho  mjini  London.

Pamaoja   an  mambo  mengine sehemu  kubwa ya  aziara  ya Zuma nchini  Ujerumani  imehusu   mgogoro wa  Zimbabwe  • Tarehe 22.04.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DmHP
 • Tarehe 22.04.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DmHP
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com